Imeelezwa kuwa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Wilfred Kidau amefutwa kazi, zilienda taarifa kwenye mitandao kuwa Kidau kajiuzuru lakini si kweli ila ameachishwa kazi.
Klabu ya Yanga SC iliwasilisha mapendekezo yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikitaka Mtendaji huyo wa TFF afutwe kazi Ili wao waweze kucheza mchezo wa dabi na Simba.
Yanga waligoma kucheza dabi mpaka pale Kidau kubwaga manyanga, hatimaye Mtendaji huyo ameondoshwa kwenye taasisi hiyo kubwa nchini.