Scout mkuu wa Simba SC, Mels Daalder amefikisha mezani jina la Pedro Goncalves Soarez (49) ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Angola ili kuchukua mikoba ya Fadlu Davids
Pedro Soarez ni miongoni mwa makocha 4 wanaowaniwa na Simba SC ili kuchukua nafasi ya kudumu kwa baadae na mpaka sasa makocha wengine 3 ni Benni McCarthy ambaye ni kocha mkuu wa Kenya, Romuald Rakotondrabe ambaye ni kocha mkuu wa Madagascar na Ahmad Ally ambaye ni kocha mkuu wa JKT Tanzania lakini bado orodha inaendelea kuletwa mezani.