KIKOSI cha Simba SC kimeondoka mchana wa leo Jijini Dar es Salaam kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Gaborone United Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa wa Botswana Jijini Gaborone.
Timu hizo zitarudiana Jumapili ya Septemba 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Simba Bhora ya Zimbabwe na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini.