Mchezaji soka wa Ecuador Jonathan Gonzalez ameuawa kwa kupigwa risasi ikiwa ni mauaji ya tatu ya katika nchi hiyo ya Amerika Kusini tangu mwanzoni mwa Septemba.
Mamlaka ilisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 aliyepewa jina la utani “Speedy” Gonzalez alipata majeraha ya risasi katika shambulio ndani ya nyumba katika jimbo la Pwani la Esmeraldas, ambalo linapakana na Colombia.
Polisi hawakutaja sababu za uhalifu huo.
Mwaka huu wachezaji wawili wa timu ya daraja la pili ya Exapromo Costa FC, Maicol Valencia na Leandro Yepez, walipigwa risasi katika shambulio la silaha katika mji wa Pwani ya Kusini Magharibi wa Manta mnamo Septemba 10.