Kuwa na mchezaji aina ya Naby Camara kwenye timu kuna faida kubwa mno sababu anakupa kitu kikubwa sana na Kocha Anaamua Amtumie kwenye nafasi gani kutokana na uzito wa mechi.
Kingine tayari kashacheza kwenye ligi ya Tunisia moja kati ya ligi bora na ya ushindani sana
Msimu uliopita alienda Qatar kupiga mipesa yake ila akaja kugundua kwa umri wake bado anahitaji kucheza ligi ya ushindani na chaguo lake limekuwa Simba SC.
Sifa Kubwa ya Camara ni Kupiga Pass zinazovunja Muundo wa Timu Pinzani, Mwepesi wa Kusoma Uhatari wa Mpinzani,anafika kwenye Matukio kwa wakati sahihi.