Kocha Nasreddine Nabi amezungumza kuhusu kwanini amechukua uamuzi wa kuondoka Kaizer Chiefs.
"Kutengana kwangu na Kaizer Chiefs ilikuwa makubaliano ya pande zote mbili na uongozi wa klabu, kufuatia uzoefu wenye mafanikio na changamoto.
Kwa sasa, nahitaji muda wa kupumzika, kuzingatia zaidi familia yangu, na kufuatilia afya ya mke wangu, ambayo imenihitaji kuwa karibu naye katika kipindi kilichopita,
"Ni kweli klabu kadhaa kubwa za Afrika na Uarabuni zimewasiliana nami, lakini sitaingia kwenye mazungumzo yoyote kwa wakati huu, kipaumbele changu ni kutojihusisha na
mpira kwa muda na kupumzika.
Nadhani hii imeweka rekodi sawa kwa wale ambao walikuwa wanamhusisha Nabi kuja Tanzania.