Klabu ya Coatal Union ya mkoani Tanga imeingia mkataba wa Mashirikiano ha kampuni ya “MO” ambapo kampuni hiyo itaidhamini klabu hiyo kupitia bidhaa zake.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya Metlgroup, Fatemagdewj amesema “Tunajivunia kushirikiana na Coastal Union FC - kuunga mkono vipaji vya nyumbani na kuleta maendeleo ndani na nje ya uwanja. Ushirikiano huu ni hatua mbele kwa michezo na biashara. Pamoja tunang’aa!”