Klabu ya Simba SC ipo hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Kocha wa Timu ya Taifa ya Madagascar, Romuald Rakotondrabe .
Kocha huyu ambaye alifika Fainali ya CHAN mwaka huu, tayari amekubaliana na Simba kuhusu maslahi binafsi, hivyo muda wowote kuanzia sasa anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC.
Awali, Simba walikuwa wanavutiwa na makocha Miguel Gamondi (Singida Black Stars) na Nasreddine Nabi, lakini kutokana na ugumu wa upatikanaji wao, uongozi umehamia kwa Rakotondrabe.