TIMU ya KMC imeanza vyema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji jiioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Daruwesh Saliboko akimtungua kipa mpya wa Dodoma Jiji FC, Ally Salim Juma Khatoro aliyesajiliwa kutoka Simba SC.