Muda wowote taarifa kamili ndani ya Simba SC zitatolewa kwamba Fadlu David's raia wa Afrika Kusini ameondoka kwenye kikosi hicho na sababu ikiwekwa wazi kutokuwa na imani na usalama wake.
Fadlu alitaka kusalia kikosini lakini hana Imani na usalama wake baada ya kusikia malalamiko toka kwa baadhi ya viongozi wa Simba.
Raja Casablanca ya Morocco inatajwa kumchukua na hivi karibuni watamtambulisha, ila taarifa za ndani zinasema kwamba Juma Mgunda ambaye anainoa Namungo FC anaweza kuchukua nafasi yake akisaidiana na Seleman Matola ingawa pia Jamhuri Kihwelu "Julio" naye akitajwa