Anaitwa Mohamed Doumbia (26) ukipenda muite “Midfield Pimper” hii ni kutokana na uwezo wake wa kucheza kwenye maeneo finyu,kupiga mashuti ya mbali yenye usahihi na akili ya kutengeneza nafasi kwa wengine.
Ni Kweli Pacome kafunga bao la ushindi ila kwangu mimi Doumbia ndo Man Of the Show.
Kipindi cha kwanza Yanga walikosa ubunifu,uthububu na ile pasi ya mwisho ya kuifungua safu ya ulinzi ya Simba.
Kipindi cha Pili Folz akaona Siyo kesi akamwambia Doumbia zama ndani na hapo kila kitu kilibadilika,Pacome,Mzize,Maxi na Ecua wakaanza kupewa pasi za upendo kwenye maeneo hatari.
Kitu kingine Nimegundua Doumbia ni “Pressing machine” jamaa ana-press Kwan akili sana,halafu akiiba mali anaachia pasi ya upendo.