Klabu ya Raja Club Athletic ya Nchini Morocco imethibitisha kumteua mkufunzi Fadlu Davids kama kocha mkuu mpya klabuni hapo akichukua mikoba ya Lassad Chabbi aliyetupiwa virago.
Fadlu Davids ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Raja AC chini ya kocha mkuu Josef Zinnbauer na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Botola Pro bila kupoteza (unbeaten) na sasa anarejea klabuni hapo kama kocha mkuu.
“Uteuzi wa Fadlu Davids kukiongoza kikosi cha kwanza cha Raja umetokana na ujuzi wake wa awali wa klabu, ambao unamfanya kuwa mtu sahihi wa kuimarisha mshikamano wa kikundi na kuiongoza Raja Club Athletic kufikia malengo yake ya kimichezo na kitaasisi.” — imesema sehemu ya taarifa ya Raja AC.