Imebainika kwamba Yanga umeamua kumzuia mshambuliaji wake hatari mzawa Clement Francis Walid Mzize asijiunge na vilabu vya Qatar Stars FC, Esperance, Wydad Casablanca na Al Masry na kutaka aendelee kuichezea Yanga.
Siri zimevuja kumbe Yanga inataka kumfanya Mzize awe mchezaji ghali nchini kwa mzawa kama ilivyo kwa Feisal Salum Feitoto wa Azam FC ambaye ndiye mchezaji ghali kwa sasa.
Yanga imemtengea shilingi milioni 45 kwa mwezi kama mshahara wake na akiwa mzawa pekee kulipwa mshahara mkubwa kwenye kikosi cha Yanga lakini atakuwa mchezaji wa pili mzawa hapa nchini kulipwa fedha nyingi.
Feitoto anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa kwani analipwa shilingi milioni 50, Mzize kwa sasa analipwa shilingi milioni 15 na ataongezewe mkataba hivi karibuni akilipwa shilingi milioni 45.