Yanga imepanga kutambulisha jezi zake mpya za msimu ujao siku ya kesho, Jumapili, Agosti 24, 2025.
Utambulisho huo wa jezi mpya za Yanga utafanyika siku tatu kabla ya uzinduzi wa jezi za watani wao wa jadi, Simba ambao utafanyika Agosti 27, 2025.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe akizungumza na vyombo vya habari, amesema kuwa uzinduzi wa jezi hizo utaenda sambamba na uuzaji wake.
"Kesho tunakwenda kuzindua Jezi zetu za ligi msimu wa 2025/26, Uzinduzi huu utafanyika kesho saa 6 mchana. Uzinduzi huu utaambatana na kuuza jezi hizi na ndiyo maana tumekuja na Kauli ya 'Tunazindua na Tunauza'," amesema Kamwe.