Tanzania imehitimisha safari yake kwenye robo fainali ya michuano ya CHAN baada ya kupoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Morocco, bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 66 na Oussma Lamlioiu akimalizia pasi ya Youssef Belammari na kuipeleka Morocco hatua ya nusu fainali.
Licha ya kutolewa, hii imekuwa ni historia mpya kwa Tanzania kwani ndiyo mara ya kwanza kufika hatua ya robo fainali tangu kuanza kushiriki michuano hii ikionesha maendeleo makubwa ya kikosi cha Taifa Stars.