Awali mamlaka za soka ziliwambia Simba na Yanga kuwa ngao ingeweza kuchezwa kati ya tarehe 11-14 ila badae ratiba ikabadilika na mechi kupelekwa tarehe 16/09/2025.
Now Simba wanasema mechi ikichezwa tarehe 16 wao hawatapata muda wa kujiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya Gaborone Utd ya Botswana.
Ikumbukwe mechi hiyo itapigwa tarehe 20/09/25 hivyo Simba wakimaliza ngao tarehe 16 kesho yake tarehe 17 watatakiwa kusafiri 3,411 km kwenda Gaborone kisha tarehe 20 kucheza mechi kubwa na ngumu kitu ambacho kwao kinawawia kigumu.
Wao Yanga wako tayari kucheza ngao ya jamii coz mechi yao ya kimataifa ni tarehe 21 hivyo watapata siku tatu za kupumzika…..ila wao Yanga wanasema tofauti na tarehe 16 “HAWACHEZI”