KLABU ya Simba Sc imetangaza kuwa Sherehe za Simba Day kwa mwaka 2025 zitafanyika Septemba 10, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Siku hiyo maalumu kwa Wanasimba ambayo hufanyika kila mwaka ni mahususi kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya.