“Kusema ukweli ukijaribu kuangalia ratiba imekuwa ngumu Sana maana ratiba ya Ngao ni tarehe 16, kuanzia hapo tutakuwa na Siku tatu au nne inabidi tucheze mchezo wa ligi ya mabingwa Botswana, na kama unavyojua utaratibu wa kusafiri Botswana Huwa ni magumu sana na mara nyingi Huwa tunaenda na Ndege ya kukodi kuepusha usumbufu”
Lakini ukijaribu kuangalia ucheze mechi tarehe 16, hapo hapo inabidi upumzike , halafu usafiri na baadae kati ya tarehe 19 au 20 ucheze Mchezo Unaweza kuona ni kwa Kiasi Gani ni vigumu”
“Kama Mchezo utakuwa tarehe 20 angalau naona Kuna namna tunaweza kukimbizana na mambo lakini kama wenyeji wetu watachagua tarehe 19 basi ratiba itazidi kuwa ngumu zaidi”
Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally akizungumza na E fm Leo.