Klabu ya Dodoma Jiji ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya beki kisiki Vedastus Masinde akitokea TMA Stars ambaye kwa sasa ni mchezaji huru,mazungumzo yanakwenda vizuri baina ya pande zote.
Masinde pia anawaniwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba SC hivyo wakati wowote beki huyo atajiunga na timu moja kati ya hizo mbili.