Nyota wa Tanzania (Twiga Stars) Clara Luvanga amekuwa gumzo nchini Hispania baada ya kufanikiwa kufunga magoli matatu (hat-trick) katika mchezo wa kirafiki baina ya klabu yake Al Nassir dhidi ya klabu ya Real Betis inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.
Katika mchezo huo ambao klabu ya Al Nassir ilishinda magoli 5 - 1 dhidi ya Real Betis, Clara alifunga magoli 3 (hat-trick).
Kwasasa klabu ya Al Nassir ipo Hispania kwaajili ya kuandaa michuano ya msimu mpya.
"Baada ya mchezo huo viongozi wa klabu ya Real Betis walishangazwa na ubora wake na kujaribu kufanya maongezi nae lakini hawakufanikiwa baada ya viongozi wa Al Nassir kumuondosha haraka Clara eneo la tukio" kiongozi wa Clara.
Katika mchezo huo walikuwa viongozi wa klabu zingine ambao nao kwa haraka wameitafuta usimamizi wa Clara kuulizia huduma yake.
Clara bado amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Al Nassir na chaguo la kwanza la uongozi wake ni kumaliza mkataba huo kisha kufungua milango kwa timu nyingine.