CHADEMA wameiandikia FIFA barua rasmi ya malalamiko dhidi ya Klabu ya Yanga, wakidai kuwa timu hiyo inaushirika wa karibu na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Barua hiyo imetiwa saini na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora wa chama hicho, ambapo wameeleza masuala kadhaa ya msingi kuhusu uhusiano huo.
Katika barua hiyo, CHADEMA wameomba FIFA kufanya uchunguzi wa kina juu ya ushiriki wa Yanga katika masuala ya kisiasa. Wamesema hatua hiyo ni muhimu ili kulinda misingi ya mpira wa miguu ambayo haipaswi kuhusishwa moja kwa moja na siasa.
Aidha, chama hicho kimetaka FIFA ichukue hatua kali mara moja endapo itabainika kuwa Yanga walihusiana na siasa, siyo klabu pekee bali pia viongozi wake wawajibishwe kwa mujibu wa taratibu na kanuni za FIFA.
Vilevile, CHADEMA wamehimiza kuzuia kabisa ushirikiano kati ya soka la Tanzania na masuala ya kisiasa ili kulinda hadhi ya mchezo huo. Wameongeza kuwa wako tayari kuwasilisha ushahidi wowote pale ambapo FIFA itahitaji, ili kuthibitisha malalamiko yao.