Kakolanya mbioni kutua Mbeya City

Aliyewahi kuwa mlinda mlango wa Tanzania Prisons,Young Africans,Simba,Fountain gates (Zamani Singida Fountain gates) na Namungo,Beno Kakolanya anatajwa kuwa katika mipango ya Mbeya City kuelekea msimu 2025/26.

Beno ni miongoni mwa walinda milango bora kuwahi kutokea aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Tanzania katika michuano ya AFCON 2023 iliyofanyika Ivory Coast.