"Albamu yangu ya NJE YA BONGO nilifanyia Nje ya nchi mwaka 1999, na ndio albamu yangu ya kwanza kuisambaza mwenyewe.
Big up kwa Mzee Kitime maana ndiye alinisaidia kusambaza albam yangu ya kwanza kabla ya albamu ya pili na ya tatu hazijachukuliwa na promota Mutta.
Baada ya kutoridhika na mwenendo mzima wa biashara niliamua kuisambaza mwenyewe.
Sasa, nikiangalia kila wanao-duplicate (durufu) ni wadosi, mahali pekee ambapo ningeweza ku-duplicate ni CHAMUDATA (Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania)
Wao walikuwa na sponsorship kutoka Norway chini ya Mzee John Kitime akiwa kama Katibu, pale walikuwa na studio na chumba kwa ajili ya ku-duplicate tapes.
Nilimfuata Mzee Kitime nikamwomba ni-duplicate albamu yangu, akasema b'ana ili uwe mnufaika lazima uwe member.
Wakati huo hatukuwa na Chama cha Rap ilibidi mimi niwe Mwanachama wa CHAMUDATA!
Kwa hiyo, mimi nimewahi kuwa member wa CHAMUDATA, big up kwa brother Kitime kwa sababu yote hii alikuwa anatafuta namna ya kunisaidia." Joseph Mbilinyi, Sugu.