Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Les Aigles du Congo mabingwa wapya DRC

TIMU ya FC Les Aigles du Congo (Eagles of Congo) ya Kinshasa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ijulikanayo kama Linafoot kwa mara ya kwanza katika historia yake baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na TP Mazembe Ijumaa ya jana (Juni 27, 2025) Uwanja wa Kamalondo, Lubumbashi.

Beki Heltone Kayembe alianza kuifungia Aigle du Congo ‘Des Samourais’, (The Samurai) dakika ya 35 akimtungua kipa Baggio Siadi Ngusia, kabla ya Patrick Mwaungulu kuisawazishia TP Mazembe dakika ya 47 akimtungua kipa Nathan Dibu kufuatia kazi nzuri ya Patient Mwamba.

Kwa matokeo hayo, Aigles du Congo inayofundishwa na Kocha wa zamani wa Tabora United, Anicet Kiazayidi inamaliza na pointi 35 kileleni mwa Linafoot ikifuatiwa na FC Saint Eloi Lupopo ya Lubumbashi pia yenye pointi 33 baada ya mechi 16 kwenye ligi ya timu 12 na zote zinafuzu Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Timu ya AS Maniema iliyomaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake 32 inakwenda Kombe la Shirikisho Afrika katika msimu ambao umekuja na mageuzi makubwa katika Linafoot, kwani hata kigogo mmoja wa kihistoria, iwe Mazembe, AS Vita Club wala DC Motemba Pembe aliyepenya nafasi tatu za juu.

TP Mazembe ya Kocha Msenegal, Lamine N'Diaye, waliokuwa mabingwa watetezi, wamemaliza nafasi ya nne kwa pointi zao 30 nyuma ya Motema Pembe iliyovuna pointi 31.

FC Les Aigles du Congo ni klabu iliyoanzishwa na Mfanyabiashara na Mwanasiasa, Vidiye Tshipanda Tshimanga mwaka 2023 yenye maskani yake Jjini Kinshasa, ambaye aliinunua klabu ya Jeunesse Sportive de Kinshasa maarufu kama JSK na kuibadili jina.

Kisiasa Vidiye Tshipanda Tshimanga (48) ni Mshauri wa Rais wa DRC, Felix Tshisekedi Tshilombo juu ya masuala
maalum a ya kimkakati.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa