Iliniuma sana Prince Dube kuhama Azam FC kwenda Yanga- Zakazi

Afisa Habari wa klabu ya Azam FC Zackaria Zakazi " Zaka Zakazi" amesema hakuna kitu kinachomuuma kama mchezaji Prince Dube aliyekuwa Azam FC kuhamia Yanga.

"Nilimuita mwanangu jina la Prince kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga mwaka 2021 halafu Prince Dube akafunga goli karibu na katikati ya uwanja,jambo lililonifurahisha sana ndio maana nikasema kwa heshima hiyo nimpe mwanangu jina lake"

"Kwa sasa nimembadilishia jina kwa sababu sifurahii tena kumuita Mwanangu Prince tangu Prince Dube alipoondoka Azam"
.
ZAKA ZAKAZI,Afisa Habari wa Klabu ya Azam FC.

Zakazi akiwa na Dube aliyevaa jezi ya Azam