Gibrili Sillah kuongeza mkataba Azam FC

Azam FC na Gibrill Sillah watakaa mezani mwezi wa 4 (siku 2 zimesalia) kujadili hatma ya Mchezaji huyo ambaye mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa msimu huu 2024/25.

Sillah aliuomba Uongozi wa Azam FC umuache mpaka itakapofika mwezi wa 4 mwaka huu ndipo afanye maamuzi, alitaka muda wa kuutumikia mkataba wake wa sasa na hakutaka kufikiria chochote kingine.

Kuna timu 2 za Ulaya (Ufaransa na Ubelgiji) ambazo zinamuhitaji Gibrill Sillah, lakini pia Wydad Casablanca nao pia wameshafanya mawasiliano na Wakala wa Sillah.

Hakuna timu yeyote ya Tanzania ambayo imeshafanya mawasiliano na Gibrill Sillah wala Wakala wake.