Yanga yaishusha kileleni Simba
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imechupa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo baada ya kuilaza Kagera Sugar ya Bukoba mabao 4-0 katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 42 ikicheza mechi 16, ikiishusha Simba yenye pointi 40.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize dakika 31, Mudathir Yahya dakika ya 60, Pacome Zouzoua (penalti) dakika ya 78 na Kennedy Musonda dakika ya 86.
Hata hivyo Stephanie Aziz Ki alikosa penalti ambapo jumla ingekuwa bao 5, kesho Tabora United wataikaribisha Simba uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora