STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI
Na E xipedito Mataruma, MBEYA
SIMBA SC imeshindwa kupata saini ya mshambuliaji wa Prisons ya Mbeya Jeremia Juma Mgunda mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga Juma Mgunda.
Jeremia Juma mmoja kati ya washambuliaji hatari waliobuka msimu uliopita, alifanikiwa kupachika mabao 14 akiwa nyuma ya Mzimbabwe Donald Ngoma wa Yanga.
Mchezaji huyo ambaye amepanda kwa kasi msimu uliopita yupo tayari kutua Simba lakini kikwazo ni dau dogo linalotaka kutolewa na klabu hiyo ya Simba.
Akizungumza na mtandao huo mshambuliaji huyo wa timu ya Prisons amesema yupo tayari kuichezea Simba msimu ujao lakini sio kwa kiasi kidogo cha pesa ambacho wanataka kumpa.
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 14 msimu uliopita na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ameiambia Mambo Uwanjani kama Simba wamepanga kumpa shilingi Mil 20 hayupo tayari na ni vyema akabakia Prisons ili aendelee kubaki kwenye ajira yake ya uaskari Magereza.
"Bado naendelea kuzungumza na viongozi wa Simba lakini tatizo linalofanya tushindwe kufikia muafaka ni dau ambalo wananitajia dogo la milioni 20, wakati hizo pesa hata Tanzania Prisons nazipata kama watashindwa nitaendelea kubaki jeshini kuliko kuacha ajira ya kudumu kwenda huko ambapo siku chache wanaweza kunitema", amesema Jeremia Juma ambaye aliwahi kuitwa Taifa Stars.
Jeremia amesema kwa sasa anatazamia kuongeza mkataba mpya na timu yake ya Prisons ingawa Azam FC nao wameonyesha nia ya kumchukua