Wakala wa Tshabalala adai timu mbili zinamtaka
Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Simba Mohamed Hussein kupitia kwa wakala wake Carlos Mastermind ameweka wazi kuwa kuna klabu mbili kutoka nje ya nchi zinazoitaka saini ya nyota huyo.
" Kuna klabu ya Afrika Kusini imetualika kufanya mazungumzo.Kuna klabu ya Libya imeonyesha kumtaka. Kama uongozi wa mchezaji hatujakaa naye kujua mpango wake ni upi lakini tutakaa, "
Carlos Mastermind, Msimamizi wa Nahodha wa Simba Sc Mohamed Hussein 'Tshabalala