Tutajiita MC KenGold- Morrison
Winga mpya wa Klabu ya KenGold Bernard Morrison Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameanza kutamba mapema kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa Siku ya Jumatano. Morrison amechapisha ujumbe unaosema;
“Jumatano tutabadilisha tu jina letu kuwa “MC KENGOLD” ili tupate matokeo mazuri dhidi ya utopolo. Kwa sababu wanaogopa majina yanayoanza na MC” – Morrison