Mabilioni ya Waarabu, kumrudisha Feitoto, Yanga
Klabu ya Young Africans inatajwa itapokea kiasi kikubwa cha fedha watakapofanya biashara ya kuwauza Clement Mzize na Aziz Stephane Ki mwisho wa msimu huu.
Kiasi watakachopata wanao uwezo wa kubisha hodi tena pale Chamazi wakamrejesha Feisal Salum halafu wakamsainisha na Djibril Silla ambaye inatajwa amegomea ofa ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia Azam Complex.