Fadlu: Simba imebebwa na mechi za kimataifa
Kocha mkuu wa timu ya Simba Sports Club Fadlu David's amesema kwamba michezo ya kimataifa imekuwa na faida kubwa sana kwake na wachezaji wake.
Fadlu David's ameongeza kwamba, safu yake ya ulinzi imetoka kwenye kufanya makosa ya kitimu na kubaki na makosa ya mchezaji binafsi.
Tatizo hilo nalo hakuliona katika michezo hii miwili iliyopita, Kombe la Shirikisho,na CRDB Federation Cup.