Yanga yafufua matumaini ya kucheza robo fainali Ligi ya mabingwa
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga SC usiku huu imefufua matumaini yake ya kutinga robo fainali baada ya kuilaza Al Hilal bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliofanyika Mauritania.
Bao pekee lililowapa ushindi Yanga limefungwa na Stephanie Aziz Ki dakika ya 06, kwa matokeo hayo Yanga sasa imefikisha pointi 7 ikiendelea kukaa nafasi ya tatu lakini inakuwa na matumaini ya kusonga mbele endapo itaifunga MC Alger.
Ikumbukwe Yanga itarudiana na MC Alger katika uwanja wake wa nyumbani wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Al Hilal inaongoza kundi lao H ikiwa na pointi 10 wakati MC Alger inapointi 8, Yanga pointi 7 na TP Mazembe inashika mkia na pointi 2.