Yanga yafufua matumaini Afrika
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika Yanga SC imefufua matumaini ya kuvuka robo fainali baada ya kuichapa TP Mazembe ya DR Congo mabao 3-1 uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 4 na kwa vyovyote imefufua matumaini yake ya kutinga robo fainali, Alouane Tatu dakika ya 15 alifunga bao kwa mkwaju wa penalti.
Lakini Clement Mzize dakika ya 32 alisawazisha bao hilo, Stephanie Aziz Ki dakika ya 55 aliipatia bao la pili kabla ya Mzize dakika ya 59 kufunga la tatu