Tabora United yaiwinda Simba
KOCHA Mkuu wa Tabora United, Anicet Kiazayidi amesema maandalizi kuelekea mchezo wa simba yanaendelea vizuri, kuhakikisha wanaifunga ili kupata pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
-
Tabora United ni wenyeji wa mchezo huo na wameahidiwa kiasi cha sh million 50 endapo watashinda mechi yao dhidi ya Simba itakayochezwa jumapili, Februari 2, uwanja wa Al Hassan Mwinyi, Tabora.
-
Amesema wachezaji wote wamewasili kambini hata wale wapya waliosajiliwa dirisha dogo wapo tayari dhidi ya wekundu hao na sasa wapo tayari kuzisaka alama hizo muhimu.
-
“Hautakuwa mchezo rahisi, Simba ni timu kubwa inaongoza ligi lakini pia, imefanya vizuri katika michuano ya kimataifa, wana wachezaji bora, tutatumia madhaifu yao kutafuta alama tatu katika mchezo huo,” amesema.
-
Kiazayidi amesema ana imani wachezaji watafuata maelekezo yake na kupambana katika mchezo huo kwa ajili ya kutafuta alama muhimu kufikia malengo yanayotarajiwa na viongozi kwa kuzifunga timu zote za Dar es Salaam.
-
Tabora United iliifunga Yanga na kuzawadiwa kiasi cha sh million 20 na kisha wakapewa sh milioni 10 baada ya kuifunga Azam FC kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania.