Tabia Batamwanya anyoosha mikono hataki bifu na mtu

Staa wa muziki wa dansi Tanzania Tabia Batamwanya ameandika katika kurasa yake ya Facebook akidai kwamba amejifunza mengi kuhusu vifo vya mara kwa mara vya mastaa wenzake hivyo hataki malumbano na mtu.

"Nimejifunza kitu kutokana na hii misiba ya ghafla ghafla na kuanzia mwaka huu sitaki bifu na mtu na sitaki kuchukiana na mtu na wala sitaki kuchambana na mtu.

Na kama kuna mtu ananichukia basi yeye aendelee kunichukia tu maana mtu unakua na roho mbaya utafikiri imezaliwa na nyoka mimi najua kwenye matatizo watu hata kama walikua wanachukiana basi zile tofauti zinatowekaga.

Na kuanza kufarijiana jamani tupendane maana sisi waislamu ukifa na kinyongo ni zambi kubwa sanasana" niwatakie mwaka mpya mwema", anaandika Tabia Batamwanya staa wa muziki wa dansi Tanzania


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA