Simba yamzuia Miquissone kwenda KenGold

Imebainika kwamba kukosekana kusajiliwa kwa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa nchini Msumbiji Luis Miquissone kwenye Klabu ya KenGold inayoshiriki Ligi Kuu bara, Simba SC imehusika.

Taarifa zisizo na shaka ambazo Mambo Uwanjani Blog imezipata kwamba Simba SC wametia mkono na kumwambia Miquissone asikubali kujiunga na KenGold kwani ni timu ndogo sana na itaharibu heshima yake.

Licha kwamba Bernard Morrison amejiunga na Klabu hiyo inayoshika mkia, lakini Miquissone ni mchezaji mkubwa aliyejijengea heshima kubwa.

Simba wamemwambia Miquissone aendelee kucheza UD Songo na kama akiongeza bidii anaweza kurejea Simba au Yanga timu kubwa na sio KenGold




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA