Simba SC yaifuata CS SFaxien Tunisia
Kikosi cha wachezaji wa Simba SC leo hii wameanza safari kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya CS SFaxien mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika.
Wakiambatana na kocha wao mkuu Fadlu Davids, Simba SC wanategemewa kupata ushindi ugenini ili kuweka hai matumaini yao ya kufika robo fainali.