Rigobert Song aula Afrika ya Kati
Aliyekuwa kocha mkuu wa Cameroon, Rigobert Song ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Uteuzi wa Song umekuja katika wakati muhimu kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), timu inayokabiliana na matokeo mabaya katika mechi za kufuzu AFCON 2025 na kwa sasa inashika nafasi ya nne katika kundi lao la kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026.