Rasmi: Baleke amalizana na Namungo FC
Klabu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi inayoshiriki Ligi Kuu bara imekamilisha usajili wa mkopo wa mwaka mmoja mshambuliaji Jean Othos Baleke kutoka Yanga SC.
Mshambuliaji huyo aliyedumu Yanga kwa nusu msimu hakuwa na maelewano na makocha wa timu hiyo na kufikia hatua ya kumpiga benchi.
Hata hivyo Baleke alibahatika kufunga bao moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Coastal Union.
Mbali ya kuichezea Yanga, Baleke aliwahi kuichezea Simba SC, ingawa mpaka sasa ni mchezaji wa TP Mazembe ya DR Congo.