Nyota wa Yanga azua jambo Ethiopia
Nyota w Klabu ya St. George ya Nchini Ethiopia ambaye amewahi kuitumikia Young Africans SC Gift Fred, amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikielezwa kuwa amesimamishwa na klabu yake kutoka na masuala ya Utomvu wa nidhamu.
Akiandika katika mtandao wake wa kijamii wa "X", ameeleza kuwa kinachomfanya kutoonekana uwanjani ni majeraha ambayo aliyapata Mwanzoni mwa mwezi wakumi na hivi sasa yuko katika hatua za mwisho ili kurejea uwanjani.