Nyosso aibukia Championship
Beki wa zamani wa Simba SC Juma Said Nyosso ameibukia kwenye kikosi cha timu ya Geita Gold ya Geita inayoshiriki Championship.
Nyosso anaungana na nyota mwingine wa zamani wa Simba, Elius Maguri, Nyosso pia amewahi kuchezea Kagera Sugar.
Geita Gold inaweza kurejea Ligi Kuu bara msimu ujao kwani inakamata nafasi ya pili nyuma ya Mtibwa Sugar inayoongoza.