Nassor Kapama huyoo Fountain Gate
Kiungo mshambuliaji wa Kagera Sugar, Nassor Kapama amejiunga na Fountain Gate FC.
Kila kitu kimekamilika na tayari amejiunga na kikosi kwaajili ya maandalizi kuelekea mechi ya Jumapili dhidi ya Yanga SC.
Kama atacheza Jumapili basi atakuwa amecheza mara mbili dhidi ya Yanga SC kwenye mzunguko mmoja wa ligi (duru ya kwanza).
Kapama alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kwenye game ya Kagera Sugar Vs Yanga SC msimu huu...