Mchambuzi Azam TV adai marefa wa CAF wanaibeba Simba na si Yanga
Aliyekuwa Mchambuzi wa masuala ya soka pale AZAM TV, Dominick Salamba amefunguka kuwa anashangwaza namna waamuzi wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) wanavyopambana kuibeba Simba kuliko Yanga
.
“Kinachoshangaza ni kwamba pamoja na utandawazi wa sasa, kwanini waamuzi wa CAF wanafanya makosa mengi? Inafikirisha sana ukitazama mechi za Simba marefa wanakuwa upande wao, lakini ukitazama mechi za Yanga inaumiza sana ni kama huyu aliyekataa penati halali la Yanha dhidi ya MC Alger juzi.
.
Aliwaza nini kutoweka penati na mchezaj kashika ndani ya boksi? Picha za marudio zinaonyesha alishika mpira. Na sheria iko wazi. Kama umeshika kwenye boksi ni penati. Ukikataa na timu ikatolewa kama vile inaumiza sana.”