Mbosso aamua kumtoa mdada mwenye kipaji cha muziki
Msanii wa muziki kutoka WCB, Mbosso ameacha Watanzania wakiwa na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu msichana mmoja aliyeonesha kipaji cha ajabu cha kuimba.Lydia Bleck
Kwa njia ya ukurasa wake wa Instagram, Mbosso ameshiriki kipande cha video cha msichana huyu Kupitia insta storey yake, na kisha akaomba msaada wa mashabiki kumsaidia kupata mawasiliano yake.
Katika ujumbe wake, Mbosso alisema, "Naomba msaada wa kupata mawasiliano ya huyu dada... Nataka kufanya kazi nae..
Trust me... Anakitu kikubwa sana ndani yake." Maneno haya ya Mbosso yameonyesha jinsi alivyoathiriwa na kipaji cha msichana huyu, na wengi wanaamini kuwa hii inaweza kuwa mwanzo wa safari mpya ya muziki kwa msichana huyu.
Chapisho la Mbosso limekuwa likisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, na watu wengi wamekuwa wakitoa maoni yao na kumpongeza Mbosso kwa kuungwa mkono vipaji vya vijana.
Wengine wamekuwa wakijaribu kumsaidia Mbosso kupata mawasiliano ya msichana huyu.