Mashabiki Yanga wamshangaa Mwenda benchi

Mashabiki wa klabu ya Yanga wanamuona beki mpya aliyetua hivi karibuni kutoka Singida Black Stars, Israel Mwenda mazoezini tu, lakini bado hajaweza kuruhusiwa kuanza kucheza lakini imefahamika kwamba tatizo ni winga wa zamani wa timu hiyo aliyewahi kupita pia Simba, Augustine Okrah.

Mwenda bado hajaanza kuichezea timu hiyo akiishia mazoezini tu huku kwenye mechi akiishia jukwaani tu na kuwa mchezaji mtazamaji.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni kwamba Yanga haiwezi kumtumia Mwenda hadi pale itakapomalizana na Okrah, aliyeishtaki klabu hiyo Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kufuatia kuvunjiwa mkataba aliokuwa nao.

Okrah anaidai Yanga malimbikizo ya ada ya usajili ambayo hakumaliziwa hadi alipositishiwa mkataba mwishoni mwa msimu uliopita akiitumikia kwa muda wa miezi sita.

Hata hivyo, uongozi wa Yanga unafanya juhudi za kuindoa kesi hiyo ili klabu yao iweze kuendelea na matumizi ya Mwenda na mastaa wengine ambao watasajiliwa.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA