Mashabiki Yanga walia na akina Injinia Hersi

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameshusha lawama zao kwa viongozi wa juu wa Klabu hiyo kwa kushindwa kuwa karibu na timu na kukosa kufuzu kwenye ardhi yake ya nyumbani.

Yanga iliilazimishwa sare tasa 0-0 na MC Alger Jumamosi iliyopita na kushindwa kuingia robo fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika huku mshindani wake MC Alger akisogea hadi robo fainali.

Wakiongea na mtandao huu, mashabiki hao wamedai kitendo cha viongozi wa Klabu hiyo hasa Rais wa Klabu Injinia Hersi na mfadhili wao Gharib Said Mohamed (GSM) waliachana na timu na kwenda Dodoma kwenye mkutano wa CCM.

"Viongozi wetu hawakuwa siriaz na timu zaidi ya wao kujali maslahi yao binafsi, walitakiwa kuhakikisha timu inashinda kwanza na sio kuiacha na kudili na mambo ya siasa", walisema mashabiki hao bila kutaja majina yao.

Viongozi wa Yanga wakiwa mjini Dodoma

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA