Kocha wa Yanga aanza visingizio
KOCHA mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amewema bayana kwamba Ligi ya Algeria iko juu kuliko Ligi ya Tanzania.
Hayo ameyasema baada ya timu yake kuondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika na timu ya MC Alger.
"Lazima tuwe wakweli ukali wa mechi za Ligi ya Tanzania sio kama zile dhidi ya timu za Algeria, Afrika Kusini, Morocco, Tunisia hawa Ligi zao ni kali sana, tunahitaji ukali kama wa Ligi hizo ili tushindane”, alisema Ramovic