Kilimanjaro Stars yaondolewa bila pointi kombe la Mapinduzi
Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars imeifunga timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars mabao 2-0 mchezo wa kombe la Mapinduzi na kutolewa bila kuambulia pointi yoyote.
Mabao ya Harambee yamefungwa na Boniface Muchiri dakika ya 56 na Ryan Ogan dakika ya 68.
Mchezo huo ulifanyika uwanja wa Gombani Pemba na kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars imetupwa nje kwenye michuano hiyo.