Kevin Sabato aenda kuinusuru Tanzania Prisons
Timu ya Tanzania Prisons Sc Januari 4,2025 imemsajili mchezaji Kevin Sabato Kongwe kutoka FountainGate Sc kuitumikia timu hiyo, ambayo inashiriki ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.
Timu ya Tanzania Prisons Sc imeendelea kufanya maboresho katika kikosi chake kupitia dirisha dogo la usajili na kufanya sajili za wachezaji mbalimbali kwaajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.